VIDEO: Chama apeleka zawadi kwa yatima

Muktasari:

SportPesa imetoa zawadi hiyo ya mchezaji bora wa msimu kwa klabu ya Simba baada ya mashabiki kupiga kura.

KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Clatous Chama baada ya kupewa pesa yake ya uchezaji bora wa msimu na SportPesa, amesema pesa hiyo anaipeleka moja kwa moja kituo cha watoto yatima kilichopo Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Viongozi wa kampuni ya SportPesa wakiongozwa na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Abbas Tarimba walimuomba Chama ashuke kwenye gari ndio walimpa zawadi hiyo ya Sh 1 milioni.

Tarimba amesema; "Tunakupa Sh 1 milioni kama zawadi baada ya kuwa mchezaji wetu bora uliyechaguliwa, nina imani hapa usalama upo wa kutosha kwa hiyo nakupa".

Baada ya kupokea pesa hiyo, Chama raia wa Zambia amesema "Ninawashukuru mashabiki wa Simba kwa kunichagua, uongozi pamoja na wachezaji wenzangu, zawadi hii naipeleka kituo cha watoto pale Kinondoni,"

Kwa upande wa kipa Aishi Manula amewashukuru viongozi wake kuwa bega kwa bega kwani bila hivyo wasingeweza kufika walipofika.

"Tunawashukuru bodi na viongozi kiujumla kwani bila wao tusingeweza kufika hapa tulipofika," amesema.

Kwa upande wa Yanga mchezaji bora wa msimu aliyechaguliwa na mashabiki ni kiungo Feisal Salum 'Fei Toto'