Canavaro asema Burundi ni kipimo cha kuiua Tunisia

MENEJA wa Taifa Stars, Nadir Haroub 'Cannavaro', amesema mechi yao na Burundi, itakayopigwa Jumapili ya wiki hii ni kipimo tosha kuelekea mchezo wao dhidi ya  Tunisia.

Amesema anaamini Burundi ni timu nzuri, itakayowapa taswira ya nini watakifanya katika mechi na Tunisia ya kufuzu michuano AFCON, itakayopigwa Novemba 9 (ugenini) huku marudiano  ikiwa ni Novemba 17 (Tanzania).

Cannavaro amesema wachezaji wana morali ya kutosha kuhakikisha wanashinda mchezo huo, ili kuwapa nguvu yakujiandaa vyema dhidi ya Tunisia.

"Wachezaji wana hamu kucheza mechi hiyo, ingawa kocha ndiye anajua nani atacheza kutokana na kiwango watakachokionyesha katika mazoezi yao ambayo tumeanza leo Jumanne, Agosti 6.

"Wachezaji wapo vizuri, naamini watafanya vyema ingawa tunaiheshimu Burundi ina wachezaji wazuri, hivyo naamini ushindani tutakaopata utatupa muelekeo wa mechi itakayokuwa mbele yetu,"amesema Cannavaro.

Pamoja na mazoezi hayo, amesema Simon Msuva, Nickson Kibabage na Himid Mao watawasili Alhamisi alfajiri

wakati Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu  tayari wameshawasili na wamewapa mapumziko ya siku moja kisha watajiunga na wenzao.