Buyern Munich yaweka nguvu kwa Marc-Andre ter Stegen

Wednesday March 25 2020

Buyern Munich yaweka nguvu kwa Marc-Andre ter Stegen,golikipa wa klabu ya Barcelona, Marc-Andre ter Stegen’s,Emanuel Neuer,BUYERN Munich,

 

BUYERN Munich imeripotiwa kuwa mbioni kuisaka saini ya golikipa wa klabu ya Barcelona, Marc-Andre ter Stegen’s, hii ni kutokana na majeruhi ya mara kwa mara yanayo mkumba golikipa namba moja wa timu hiyo Emanuel Neuer.

Ter Stegen’s mapema mwezi huu alikataa kuongeza mkataba huku akishinikiza anahitaji mkataba mnono zaidi utakaomfanya mchezaji wa pili kulipwa mpunga mrefu nyuma ya Lionel Messi. Kwa sasa ana umri wa miaka 27, miaka sita nyuma ya Neuer ambaye ana miaka 33, hivyo Buyern wanaweke nguvu zaidi wakiamini watamtumia kwa muda mrefu zaidi.

Taarifa kutoka ujerumani zinasema kumekuwa na mkwaruzano kati ya Neuer na Rais wa klabu ya Buyern, Franz Beckenbauer, jambo ambalo linaonyesha kuna asilimia kubwa ya Ter Stegen kuingia klabuni hapo msimu ujao. Mpaka sasa Barcelona hawaaonekani kuwa na nia ya kumpa mkataba mpya.

Advertisement