Bushoke kutumbuiza jukwaa moja na baba yake

Muktasari:

Bushoke anasema ni kitu kikubwa kwake kuwepo kwenye tamasha hilo pamoja na mzee wake, anaamini kupitia nyimbo zake ataendelea kudumisha Kiswahili kwa wasanii watakuwepo.

MWANAMUZIKI wa bongo fleva, Ruta Bushoke ni kati ya wasanii watakaotumbuiza kwenye kumbukumbu ya siku ya Nelson Mandela, itakayofanyika Julai 18, nchini Afrika Kusini.
Pia ni siku inayotambua mchango wa mwanzilishi wa Kiswahili ambaye ni Rais wa kwanza wa Tanzania, Hayati Julius Nyerere.
 Wasanii kutoka nchi mbalimbali za Afrika, watakuwepo kwenye tamasha hilo, ambapo Bushoke amealikwa pamoja na baba yake mzazi Maximillian Bushoke.
Bushoke anasema ni kitu kikubwa kwake kuwepo kwenye tamasha hilo pamoja na mzee wake, anaamini kupitia nyimbo zake ataendelea kudumisha Kiswahili kwa wasanii watakuwepo.
"Pamoja na kwamba ni siku ya kumbukumbu ya hayati Nelson Mandela ambaye ana historia kubwa ya kupigania uhuru wa Afrika Kusini, pia inampa heshima baba wa taifa la Tanzania, Nyerere kutambua mchango wake katika kukuza Kiswahili.
"Jambo lingine nafurahia kwenda kuimba na baba yangu jukwaani moja, imewahi kutokea mashabiki walifurahia sana, hivyo itakuwa siku ya tofauti kwetu,"anasema.