Burundi yaita 23 kwa Afcon, Mavugo ndani

Wednesday June 12 2019

 

Cairo, Misri. Kocha wa Burundi, Olivier Niyungeko ametangaza kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 akiwemo mshambuliaji wa zamani wa Simba, Laudit Mavugo tayari kwa fainali za Mataifa ya Afrika zitakazoanza Misri hapo Juni 21.

Burundi imeweka historia kwa kucheza kwa mara ya kwanza fainali za Afcon baada ya kunaliza wapili katika kundi lake lililoongozwa na Mali, Sudan Kusini na Gabon.

Kikosi cha Burundi kinaundwa na wachezaji nyota akiwemo mshambuliaji wa zamani wa Stoke City, Saido Berahino pamoja na Mavugo aliyeshindwa kutamba katika kikosi cha Simba.

Burundi imepangwa Kundi B itafunga kampeni yake kwa kucheza dhidi ya Nigeria hapo Juni 22, kabla ya kuzivaa Madagascar na Guinea kati ya Juni 27 na Juni 30.

Kikosi cha Burundi:

Makipa: Jonathan Nahimana, Justin Ndikumana, Arthyr Mac Arakaza

Advertisement

Mabeki: Frederic Nsabiyumva, Moussa Omar, David Nshimirimana, Ngando Omar, Christophe Nduwarugira, Karim Nizigiyimana

Viungo: Pierrot Kwizera, Gael Bigirimana, Gael Duhayindavyi, Moustapha Francis, Enock Nsabumukama, Shassir Nahimana

Washambuliaji: Fiston Abdoul-Razak, Saido Berahino, Mohamed Amissi, Cedric Amisi, Shabani Hussein, Elvis Kamsoba, Laudit Mavugo, Selemani Ndikumana.

Advertisement