Beki Stars aisubiri Yanga tu

Thursday June 27 2019

 

By Khatimu Naheka

LICHA ya kuwa na majukumu mazito na timu ya taifa nchini hapa, beki wa Lipuli, Ally Mtoni ‘Sonso’ amesema bado hajasaini mkataba wa kuichezea Yanga, lakini anasubiri hatua ya kumalizana nao kwani walishaanza mazungumzo mapema.

Akizungumza na Mwanaspoti, Sonso alisema mazungumzo yake na Yanga yalikamika muda mrefu.

Beki huyo alisema yuko tayari kujiunga na Yanga kukamilisha sehemu ya ndoto yake katika kufungua fursa zaidi za kufika mbali.

Alisema anaamini kwamba usajili wake utakamilika haraka mara baada ya kurejea nyumbani kama ambavyo wamekubaliana na mabosi wa Yanga.

“Kila kitu kipo sawa, nawasubiri Yanga wenyewe waje tumalizane. Kimsingi tulikubaliana kila kitu tukiwa nyumbani,” alisema Sonso.

“Nafikiri tukirudi nyumbani mapema jambo hili tunaweza kulimaliza kama mambo yataenda kama tulivyokubaliana,” alisisitiza beki huyo ambaye akishirikiana na wenzake waliisaidia Lipuli kumaliza katika nafasi ya sita katika Ligi Kuu Bara na pia kufika fainali ya Kombe la FA, walikopoteza dhidi ya Azam FC kupitia goli la Obbrey Chirwa. .

Advertisement

Advertisement