Beki De Ligt aenda Juventus kukamilisha uhamisho wake

Tuesday July 16 2019

 

Turin, Italia. Nahodha wa Ajax, Matthijs de Ligt leo Jumanne atasafiri kwenda Turin kwa lengo la kukamilisha uhamisho wake wa kujiunga na Juventus.

Inaaminika kuwa mabingwa wa Italia watalipa pauni 67.5milioni kwa ajili ya kupata saini ya beki huyo mwenye miaka 19, aliyeiongoza Ajax kufuzu kwa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu uliopita.

Beki huyo wa kati wa Uholanzi amekuwa akihusishwa na kutakiwa na Manchester United, Barcelona na Paris-St Germain kwa muda mrefu.

Katika misimu yake mitatu aliyocheza Ajax, amefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ‘Eredivisie’ Kombe la Dutch, pamoja na kucheza fainali ya Europa Ligi mwaka 2017.

De Ligt amefunga mabao nane katika mechi 77 alizocheza katika ligi akiwa na klabu hiyo ya Amsterdam, who he joined at the age of nine.

De Ligt ndiye nahodha mdogo zaidi kuiongoza klabu hiyo tangu Machi 2018.

Advertisement

Beki huyo ndiye aliyefunga bao la ushindi dhidi ya Juve na kuivusha Ajax kucheza nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa ambako walitolewa na Tottenham.

De Ligt alianza kuichezea Uholanzi Machi 2017, akiwa ndiyo kwanza amecheza mechi mbili tu za ligi na kikosi cha Ajax wakati huo.

Advertisement