Bayern Munich bado yamuandama Leroy Sane

Muktasari:

  • Bayern ina uhakika wa kumnasa winga huyo kutokana na kuwa uhusiano mzuri na Pep Guardiola ambaye ni kocha wao wa zamani.

BAYERN Munich imedaiwa kuwa na uhakika wa kuinasa saini ya winga mahiri wa Manchester City, Leroy Sane, 23 na kumrudisha nyumbani staa huyo wa kimataifa wa Ujerumani katika dirisha hili kubwa la uhamisho wa wachezaji.

Sane, 23 amepoteza nafasi katika kikosi cha Kocha, Pep Guardiola na mara nyingi amekuwa akitokea katika benchi na mazungumzo mpya ya mkataba baina yake na City yamekwama huku mkataba wake wa sasa ukitarajiwa kumalizika mwaka 2021.

Bayern ina uhakika wa kumnasa winga huyo kutokana na kuwa uhusiano mzuri na Pep Guardiola ambaye ni kocha wao wa zamani.

Hata hivyo, City haitamuachia kwa urahisi staa huyo iliyemnunua kwa dau la Pauni 37 milioni katika dirisha la uhamisho la mwaka 2016 akitokea Schalke 04 na itataka kiasi cha Euro 100 milioni.