Barcelona yamtosa Firmino kisa Rashford

Tuesday October 15 2019

 

Madrid, Hispania. Barcelona imefuta mpango wake wa kumsajiki nyota wa Liverpool, Roberto Firmino sasa imemgeukia mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford.

Barcelona inamuona Rashford ni bora zaidi ya Firmino aliyekuwa katika mipango yao ya awali.

Rashford alitia saini mkataba wa miaka minne wenye mshahara wa pauni 200,000 kwa wiki, lakini kinda huyo mwenye miaka 21 ameonekana bora zaidi ya Firmino.

Klabu hiyo inasaka mchezaji wa kuziba pengo la Luis Suarez na miongoni mwao yumo nahodha wa England na Spurs, Harry Kane pamoja na Kylian Mbape wa Paris Saint Germain (PSG).

Katika orodha hiyo yumo mshambuliaji wa Inter Milan, Lautaro Martinez.

Suarez (33) anajiandaa kuondoka Nou Camp katika usajili wa majira ya kiangazi msimu ujao.

Advertisement

Ingawa Barcelona ina nyota Lionel Messi, Antoine Griezmann na Ousmane Dembele, lakini inasaka mchezaji wa kuongeza nguvu katika kikosi hicho.

Majina ya mastaa wanne wanaotamba Ulaya, wapo katika rada ya Barcelona na mmoja wao atasajiliwa kujaza nafasi ya Suarez raia wa Uruguay.

Advertisement