Baby Madaha aja kivingine

Saturday June 27 2020
madaha pic

MWIMBAJI na mwigizaji mahiri nchini aliyekuwa kimya kwa muda mrefu, Baby Madaha amefichua amerudi kivingine kwenye muziki akiwa na ngoma mpya zipatazo nne.
Baby aliyeibuliwa na Bongo Star Search 2007, amesema ukimya wake ulikuwa na maana kubwa kwa kujichimbia studio akiandaa ngoma na ishu za janga la corona likamtibulia kuacihia kazi mapema, lakini kwasasa kila kitu kipo poa na mashabiki wake wajiandae kupata burudani.
Akizungumza na Mwanaspoti online  mapema leo Jumamosi, staa huyo Amore, Nimezama na Mr Deejay amesema; "Nimefanya ngoma nne katika studio za Bantu Music chini ya prodyuza, Frenkenstein, nitaangusha moja baada ya moja."
Amezitaja nyimbo hizo mpya ni 'Magufuli Love', 'Umenikoroga', 'Corozon' na 'Ni Wewe', huku akisema zote ameziimba mwenyewe kwa kuwa yeye sio muumini wa kupiga kolabu.
"Unanijua vyema tangu nikiwa Candy n Candy, napenda kupiga kazi mwenyewe na hata safari hii nimefanya nyimbo hizo mwenyewe ili kuwapa ile ladha ambayo mashabiki waliikosa kwa muda," amesema aliyewahi kufanya kazi nchini Kenya huku akitamba na filamu mbalimbali  ikiwamo ile ilitwaa tuzo Afrika ya Ray of Hope, Blessed by God, Tifu la Mwaka na Misukosuko.

Advertisement