Azam hawana shuguli ndogo, Dube moto ni ule ule

Muktasari:

Mabao mawili ya Mshamvuliaji Prince Dube na moja la kiungo Mudathir Yahya yamewafanya Azam kwenda mapumziko wakiongoza kwa bao 3-0, dhidi ya Fountain Gate ya Dodoma.

MCHEZO wa kirafiki kati ya Azam Fc na Fountain Gate, umeenda mapumziko kwa Azam kuongoza bao 3-0 uwanja wa Chamanzi Complex.

Mchezo umeanza kwa timu zote mbili kucheza kwa kujilinda zaidi na kushambulia kwa kushitikiza.

Dakika ya 13, nyota wa Azam Richard Djodi alikosa bao la wazi baada ya kubaki yeye na golikipa na kupiga shuti lililookolewa na golikipa wa Fountain Gate Mussa Webilo.

Dakika ya 24, beki wa Azam FC Bruce akangwa  alipiga krosi kutokea pembeni iliyomkuta kiungo Mudathir Yahya ndani ya boksi la 18 la Fountain Gate na kufunga bao kwa shuti baada ya mabeki wa timu hiyo kuteleza na kuanguka.

Lango la Fountain Gate lilizidi kuwa na hatari kwani dakika ya 28 Mudathir Yahya alikosa bao la wazi kwa kupaisha mpira juu.

Azam FC waliendelea kulisakama lango la Fountain Gate wakati Mshambuliaji Richard Djodi kuonekana kuwa hatari zaidi, dakika ya 29 alichezewa rafu nje kidogo ya boksi la 18 na kupewa faulo iliyopigwa na kiungo Never Tigere ikagonga mwamba.

Kutokuelewana kwa mabeki wa Fountain Gate kumewafanya wajichanganye na mmoja kunawa mpira kwenye boksi la 18 na Azam kupewa penati iliyofungwa na Mshambuliaji Prince Dube dakika ya 44 na kuwapatia azam bao lapili.

Dakika ya 45, Dube aliipatia Azam Fc bao la tatu baada ya kumalizia pasi safi iliyopigwa na nahodha wa kikosi hicho kwa leo Bruce Kangwa.

Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika Azam FC walikua wanaongoza kwa bao 3-0.