Aussems avujisha siri za Kagere

Muktasari:

Hata hivyo, Kocha wa Simba, Patrick Aussems amefichua sababu za kushindwa kupata matokeo ma-zuri na kukwama kusonga mbele kwenye michuano hiyo.

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba wameondolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mab-ingwa Afrika hatua ya awali kwa sheria ya bao la ugenini.

Simba waliaga mashindano hayo juzi baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Union Deportivo de Songo ya Msumbiji. Katika mchezo wa awali ulio-fanyika kule Msumbiji ulimalizika kwa suluhu ya bila kufungana na juzi katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Simba walikuwa nyuma hadi dakika ya 85 kabla ya Erasto Nyoni kufunga kwa penati.

Licha ya kucheza mpira mwingi na kutengeneza nafasi nyingi za mabao na kushambulia lango la wapinzani wao kwa dakika ny-ingi, ndoto za Simba kufika mbali msimu huu kwenye michuano hiyo ziligonga mwamba.

Hata hivyo, Kocha wa Simba, Patrick Aussems amefichua sababu za kushindwa kupata matokeo ma-zuri na kukwama kusonga mbele kwenye michuano hiyo.Alisema kuwa licha ya kujiamini kupita kiasi kwenye mchezo huo kutokana na rekodi ya kutopoteza mechi za nyumbani, lakini ku-kosekana kwa straika wa kucheza na Meddie Kagere kumemuangu-sha.

Alisema kabla ya dirisha la usajili wa ndani na ule CAF kufun-gwa, aliwaomba vion-gozi kusajili straika mmoja mwenye uwezo zaidi ya waliokuwepo akihofia kutokea shida ya kuwa majeruhi kwa waliokuwepo.

“Nilikuwa nataka mshambuliaji mwingine kwani niliamini inaweza kuto-kea kati ya watatu kwa maana ya Bocco, Kagere na Wilker kuu-mia nikakosa mbadala na ndio kimetokea dhidi ya UD Songo,” alisema. “Kagere alikuwa peke yake na muda wote aliwekwa chini ya ulinzi na mabeki wa Songo, Bocco ameumia na nililazimika kumpumzisha Kagere katika mazoezi ya siku mbili kabla ya mechi ili asiumie. “Faida ilikuwa upande wa Kagere kweli kutoku-umia na kuingia katika mchezo huo akiwa salama, lakini kutokufanya kwake maz-oezi kwa siku mbili huenda kulichangia kupishana na wenzake ambao walikuwa waki-fanya mazoezi siku zote.

Ilikuwa lazima tufanye hivi kwa usalama na mahitaji ya timu.”Msimu uli-opita kwenye michuano hiyo, Kagere alimaliza akiwa na mabao sita akianza kufunga katika hatua ya awali yaliyomfanya kuwa kinara wa ufungaji huku Simba ikiishia hatua ya robo fainali kwa kuondolewa na TP Mazembe.

OKWI, KOTEI WAKUMBUKWAA

ussems alisema msimu uli-opita ilikuwa furaha kwa kila mtu ndani ya timu, lakini msimu huu mambo yamekuwa tofauti huku akiwakumbuka baadhi ya wachezaji wake wa zamani.“Malengo yetu ni kufika mbali zaidi ya msimu uliopita, lakini haikuwa hivyo jambo ambalo lime-kuwa baya kwetu,” alisema.

“Msimu uliopita tulikuwa na wachezaji wa kigeni ambao walifanya vizuri kama Emmanuel (Okwi) na Juuko Murshid, Mghana James Kotei na wengineo, lakini waliondoka kutokana na mikataba yao kumalizika.“

Halikuwa jambo zuri kwa wachezaji hao waliofanya vizuri kuondoka, lakini kuna masuala ya kimaslahi na kimsingi, hivyo ilikuwa ngumu kuwabakiza