Aussems: Tutawashambulia AS Vita

Muktasari:

Aidha kiungo wa timu hiyo Haruna Niyonzima ambaye ni nahodha msaidizi amesema wanatambua ugumu wa mchezo huo lakini lengo lao ni kupata pointi tatu au moja wazidi kujikita kileleni

Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema hawatajilinda katika mchezo wa kesho bali watawashambulia Vital Club dakika zote tisini.
Aussems amesema wanatambua wanakutana na Vital Club itakayotaka kuwapa furaha mashabiki  wao baada ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Al Ahly ya Misri.
Amesema wataingia uwanjani na mpango wa kushambulia na sio kujilinda.
Aidha kiungo wa timu hiyo Haruna Niyonzima ambaye ni nahodha msaidizi amesema wanatambua ugumu wa mchezo huo lakini lengo lao ni kupata pointi tatu au moja wazidi kujikita kileleni
Niyonzima amesema maandalizi yao yamekuwa makubwa na kwamba kila mchezaji anatambua umuhimu wa mchezo huo kulingana na malengo ya timu yao.
Amesema Vita Club ni timu kubwa wanaiheshimu lakini hawawezi kuiogopa.