Aussema achekelea kuifunga Mtibwa Sugar

Friday September 13 2019

 

By DORIS MALIYAGA

KOCHA mkuu wa Simba, Patrick Aussems amefurahishwa na matokeo ingawa amesema mchezo huo ulikuwa mgumu.
Akizungumza mara baada ya mchezo huo uliochezwa uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, ambapo Simba imeifunga Mtibwa Sugar bao 2-1 kuwa wapinzani wao ni wazuri.
"Mtibwa walikuwa wazuri na wametupa wakati mgumu hasa kipindi cha kwanza lakini cha pili tulijua mambo yakawa mazuri,"alisema Aussems.
Aussems amepongeza kuwepo kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba mpya, Senzo Mazingisa ambaye ameshuhudia timu yake ikiibuka na ushindi huo mara ya pili mfululizo tangu msimu huu uanze.
"Nina furaha kuchaguliwa kwake binafsi nina furaha Simba wamefanya kitu kikubwa,"alisema Aussems.
Kwa upande wa Kocha wa Mtibwa Sugar, Zubery Katwila alisema,  Simba waliwazuia kucheza.
"Mechi ilikuwa ngumu lakini ni sehemu ya mchezo hata hivyo, mechi za mwanzoni mwa ligi huwa hivyo,"alisema Katwila.
Alisema, timu inayoanza kufungwa inakuwa hivyo na anayefanikiwa matokeo mazuri anakuwa na furaha.

Advertisement