Ati show ya Tanasha imenuka!

Wednesday February 5 2020

MPENZI wa Diamond Platinumz msupa Mkenya, Tanasha Donna ,uzinduzi wa EP DonnaTella,

 

By Thomas Matiko

Nairobi, Kenya.MPENZI wa Diamond Platinumz msupa Mkenya, Tanasha Donna kajitetea baada ya kutolewa rangi kinoma na wengi alichemsha kinoma kwenye pati ya uzinduzi wa EP DonnaTella.

Mastaa kibao wa muziki hapa nchini walihudhuria hafla hiyo katika Ukumbi wa Sarit Center Expo kwa ajili ya kumpa sapoti Jumamosi iliyopita. Hata hivyo, ukweli wa mambo ni uzinduzi wa EP hiyo haukuvutia kabisa wengi wakimtoa rangi Tanasha kwa kushindwa kujipanga.

Utumbuizaji wake ulikuwa wa kama vile mtu anayejifunza kuimba. Mara kwa mara aliimba nyimbo zake nje ya biti. Hakukuwa na mvuto wala msisimko jambo ambalo lilipelekea wengi kumtoa rangi.

Wengine walidai kuwa ili kuepuka fedheha, ndio sababu mpenzi wake Diamond Platinumz aliamua kurudi nyumbani kwao kwenye siku ya uzinduzi kwa kile walichodai kisingizio cha jambo la dharura la kifamilia.

Hata hivyo, akijibu mapigo, Tanasha kadai hakuwa na muda wa kutosha wa kujiandaa na kuahidi kujipanga vizuri zaidi wakati mwingine.

“Kwa kuwa ilikuwa mara yangu ya kwanza kufanya kitu kama kile, naaamini nilijitahidi ukizingatia nilikuwa na siku mbili tu ya kufanya mazoezi. Ila najua nilipaswa kujitahidi hata zaidi” Tanasha kajitetea.

Advertisement

Kibaya cha haya ni kuwa Tanasha alianza kutangaza suala la kuachia EP hii Septemba mwaka jana hivyo yeye kudai hakuwa amejiandaa vizuri, ni jambo la kuchekesha kama sio kushangaza.

Advertisement