Aston Villa yanukia Ligi Kuu England

Thursday May 16 2019

 

London, England. Aston Villa imebakiwa na mechi moja dhidi ya Leeds au Derby ambayo ikishinda itarejea katika Ligi Kuu England msimu ujao.

Kipa Jed Steer alikuwa shujaa wa Aston Villa, baada ya kuokoa penalti mbili dhidi ya West Bromwich Albion katika mchezo wa juzi usiku.

Tammy Abraham alifunga penalti ya mwisho iliyoipa ushindi Aston Villa wa mabao 4-3 baada ya kutoka sare ya bao 2-2.

Pia katika mchezo huo uliokuwa na ushindani, nahodha wa Albion Chris Brunt alitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 80.

Aston Villa inatarajiwa kuvaana na Leeds au Derby katika mechi ambayo itaamua timu ya kupanda Ligi Kuu itakayochezwa Uwanja wa Wembley Mei 27.

Katika hatua nyingine, Bayern Munich imetuma maombi ya kutaka saini ya winga wa Manchester City, Leroy Sane katika usajili wa majira ya kiangazi.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani, bado hajafikia makubaliano ya kutia saini mkataba mpya Man City.

Sane mwenye thamani ya Pauni 37 milioni amekuwa katika kiwango bora msimu huu.

 

Advertisement