Arsenal yaibinua Fulham mabao 5-1

Muktasari:

Ushindi huo umeisogeza Arsenal hadi nafasi ya tatu ikiwa na pointi 18 baada ya kucheza mechi 8. Man City imejikita kileleni ikiwa na alama 19 ikifuatiwa na Liverpool yenye pointi 19 huku timu hizo zikitarajiwa kucheza leo jioni.

England. Timu ya Arsenal imeibuka na ushindi mnono mbele ya Fulham wakiwa nyumbani kwao baadca ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-1.

Alexandre Lacazette aliifungia timu yake mabao mawili akifungua kapu la mabao baada ya kuziona nyavu dakika ya 29’ na kutupia jingine la pili dakik aya 49’.

Aaron Ramsey aliweka wavuni bao la tatu dakik ya 67’ wakati Pierre Emerick Aubemeyang akitupia wavuni mabao mawili dakika ya 79’ na 90’.

Ushindi huo mnono umeacha tabasamu kwa mashabiki wa Arsenal ikiimarisha katika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu England.