Arsenal, Chelsea zakomaa sura ya kazi Ligi ya Europa

Friday March 15 2019

 

Timu  mbili za Uingereza, Arsenal na Chelsea zina nafasi ya kushinda taji hilo baada ya mabingwa mara tano, Sevilla kutupwa nje ya mashindano hayo katika hatua ya 16 bora pamoja na Inter Milan.

Sevilla ilishangaza baada ya kupata kipigo cha mabao 4-3 kutoka kwa  Slavia Prague ya Jamhuri ya Czech hivyo kutolewa kwa jumla ya mabao 6-5 wakati Inter Milan ilitolewa kwa kufungwa Eintracht Frankfurt ya Ujerumani bao 1-0.

Chelsea ilitinga robo fainali ya mashindano hayo baada ya kuichapa Dynamo Kyiv ya Ukraine mabao 5-0 huku Olivier Giroud akifunga Hattrick mengine yalifungwa na Marcos Alonso na Callum Hudson- Odoi.

Mchezo wa kwanza Chelsea ilishinda mabao 3-0 hivyo kwenda hatua ya robo fainali kwa jumla ya mabao 8-0. 

Arsenal ilifanikiwa kuifunga Rennes ya Ufaransa mabao 3-0 yaliyofungwa na  Pierre-Emerick Aubameyang aliyefunga mawili dakika ya 5 na 72 na lingine likifungwa na  Ainsley Maitland-Niles dakika ya 13.

Advertisement