Anatoka Koscielny linaingia jembe lingine William Saliba, mjipange

Muktasari:

Saliba alicheza mechi 16 katika msimu wake wa kwanza huko kwenye Ligue 1 msi mu ulio pita.

LONDON, ENGLAND.HUKO Arsenal, Kocha Unai Emery anatoa kitu anaingiza kitu. Ni hivi, Mhispaniola huyo ameshapanga ni jembe gani la kununua wakati Laurent Koscielny atakapoondoka kwenye kikosi chake.

Beki huyo Mfaransa, Koscielny, ambaye umri umeshaanza kumtupa mkono anasakwa na Borussia Dortmund ya Ujerumani ikihitaji huduma yake na Arsenal inaweza kuiuzia kwa Pauni 10.6 milioni.

Hata hivyo, Kocha Emery ameshatambua mapema sana ni mchezaji gani atakuja kuziba pengo la Koscielny akiondoka kwenye kikosi chake, akimtazama beki wa kati, William Saliba, anayekipiga huko Saint-Etienne anafaa zaidi.

Beki huyo kinda, anaweza kupatikana kwa ada ya Pauni 27 milioni tu.

Mabeki wengine wa kati ambao Emery anawapigia hesabu ni Dayot Upamecano, anayekipiga Leipzig na Joachim Andersen wa Sampdoria, ambao wote bado ni makinda.

Kuhusu kinda Saliba amedaiwa kuwindwa pia na Manchester United, lakini Arsenal ndio iliyopo kwenye nafasi nzuri ya kunasa saini yake.

Saliba alicheza mechi 16 katika msimu wake wa kwanza huko kwenye Ligue 1 msi mu ulio pita.

Staa wa zamani wa Arsenal, Laur en ali mzu ngu mzia Saliba na kusema: “Anaonekana ni mchezaji mzuri sana. Ana nguvu, mrefu na anaweza kutoka na mpira nyuma na kitu kingine ni Mfaransa.”

Emery ana bajeti ndogo ya usajili, ikidaiwa ni Pauni 40 milioni tu za kusajili baada ya kikosi chake kushindwa kukamatia tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.