Ali Kiba, Diamond watunishiana misuli Instagram

Muktasari:

Ni muda mrefu sana tangu Alikiba ametangaza kuwa miongoni mwa wawekezaji walioweka hisa zao katika kinywaji cha Mofaya sasa amefunguka rasmi kuwa anatarajia kutangaza sehemu zitakapokuwa zinapatikana ikiwa ni pamoja na bei yake.

SIKU chache baada ya Naseeb Abdul 'Diamond Platnams' kuonyesha matamanio ya kufanya tamasha pamoja na msanii mwenzake Ally Saleh 'Alikiba' katika jukwaa moja nyota huyo amejibu kuwa hataweza kufanya hivyo kutokana na kubanywa na majukumu mengine na kuomba kuwa mdhamini wa tamashahilo.
Diamond Platnams mwanzoni mwa wiki alizindua redio yake mpya na tamasha la wasafi festival linalotarajia kufanyika katika maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kutoa burudani na kutangaza utalii.
Kupitia mtandao wake wa kijamii 'Instagram' Alikiba amewashukuru Wasafi kwa kumpa mwaliko huo na kuweka wazi kuwa hataweza kuudhuria kutokana na kuwa na majukumu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuinadi bidhaa yake mpya ya Mofaya katika mataifa mbalimbali.
"Hata hivyo mimi pamoja na menejment yangu hatupendi kuwaacha hivyo hivyo tunaomba kuwa wadhamini wa tamasha lenu kupitia kinywaji chetu cha Mofaya ili kuweza kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya sanaa yetu Tanzania na Afrika," alisema.

Vilevile Diamond alijibu kwenye ukurasa huo kupitia Kampuni yake ya WBC kwamba atamuagiza meneja wake akutane na Ali Kiba kuona ni jinsi gani wanaweza kufanikisha zoezi zima la udhamini