Aiyee hataki maneno mengi

Muktasari:

"Sitaki kuzungumza maneno mengi kwa sababu nataka kazi yangu ionekane kwa vitendo. Wakati wote maneno si matendo ambayo mimi nataka kuonyesha,"alisema Aiyee.

MSHAMBULIAJI wa KMC, Salim Aiyee amesisitiza hataki maneno kwa sababu yeye ni mtu wa vitendo na anarudi uwanjani kwake itakuwa ni kazi kazi tu.
Aiyee ameanza msimu mpya na klabu mpya ya KMC akitokea Mwadui FC alikumbana na mkosi kwani baada ya kusajiliwa tu, alipata maumivu ya nyonga  yakamweka nje ya uwanja kwa kipindi kirefu.
"Sitaki kuzungumza maneno mengi kwa sababu nataka kazi yangu ionekane kwa vitendo. Wakati wote maneno si matendo ambayo mimi nataka kuonyesha,"alisema Aiyee.
"Kiafya, nimepona kabisa sina kinachonisumbua, kilichobaki ni kufanya kazi yangu tu nitakapokuwa uwanjani."
Mtaalamu huyo wa kufunga mabao ya miguu na vichwa, alimkimbiza mfungaji bora wa msimu uliopita, Mnyarwanda Meddie Kagere ambaye alimaliza na mabao 23 na yeye akapachika mabao 18, huku akishika nafasi ya tatu.