Abalora mambo safi huko Ghana

Muktasari:

  • Kikosi hicho cha awali cha Ghana cha wachezaji 29 kinajumuisha makipa Richard Ofori Lawrence Ati Zigi, Felix Annan na Razak Abalora wakati mabeki ni Kassim Nuhu, Jonathan Mensah Musah Nuhu, Joseph Aidoo, Mohammed Alhassan, Lumor Agbeyenu, Harrison Afful, Baba Rahman na Andy Yiadom.


NEEMA imetua kwa kipa wa Azam FC, Razak Abalora baada ya kuteuliwa kwenye kikosi cha awali cha nchi hiyo kwa ajili ya maandalizi ya Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) huko Misri mwaka huu.

Ghana inatarajia kuweka kambi huko Dubai baadaye mwezi huu na Abalora anapata nafasi ya kuitwa kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha ‘Black Stars’ ingawa atapaswa kupambana na makipa wengine watatu ili aweze kuwemo kwenye kikosi cha mwisho kitakachokuwa na wachezaji 23 kwa ajili ya fainali hizo.

Hakukuwa na nafasi kwa winga wa Azam, Enock Atta Agyei ambaye amekuwa akiitwa mara kwa mara kwenye kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 lakini kocha Kwesi Appiah hajamjumuisha beki Yakub Mohammed ambaye naye anachezea Azam.

Pamoja na kiwango bora alichoonyesha kwenye ligi ya mabingwa Afrika na Ligi Kuu akiwa na kikosi cha Simba, kiungo James Kotei hajajumuishwa kundini kama ilivyo kwa beki wa kulia, Gyan Nicolas.

Kikosi hicho cha awali cha Ghana cha wachezaji 29 kinajumuisha makipa Richard Ofori Lawrence Ati Zigi, Felix Annan na Razak Abalora wakati mabeki ni Kassim Nuhu, Jonathan Mensah Musah Nuhu, Joseph Aidoo, Mohammed Alhassan, Lumor Agbeyenu, Harrison Afful, Baba Rahman na Andy Yiadom.

Viungo yupo Kwadwo Asamoah, Thomas Partey, Andre Ayew, Afriyie Acquah, Mubarak Wakaso, Ebenezer Ofori, Yaw Yeboah, Abdul Fatawu Safiu, Christian Atsu, Thomas Agyepong, na Samuel Owusu.

Wakati safu ya washambuliaji ameitwa kikosi Emmanuel Boateng Jordan Ayew, Majeed Waris,Caleb Ekuban na Kwabena Owusu.