AS Vita chini ya ulinzi mkali kuihofia Simba

Thursday March 14 2019

 

Dar es Salaam. Timu ya AS Vita imefanya mazoezi leo Alhamisi kwenye Uwanja wa Gymkhana jijini Dar es Salaam ikiwa ni maandalizi ya mchezo wao dhidi Simba utakaopigwa Jumamosi saa moja jioni.

Mazoezi hayo ya AS Vita yalikuwa chini ya ulinzi mkali wa maofisa wake huku waandishi wa habari wakizuia kuingia kwenye viwanja hivyo.

Jumla ya mechi nane za Ligi ya Mabingwa Afrika zinatarajiwa kuchezwa Jumamosi ili kupata timu zitakazoshindano hayo hatua ya robo fainali.

Mechi za robo fainali zimepangwa kuanza Ijumaa ya Aprili 5, huku kundi gumu zaidi likitajwa kuwa ni Kundi D..

Mechi hizo zitawakutanisha Horoya FC dhidi ya Orkando Pirates.  Pia Club Africa watakuwa wanawakaribisha Ismaily.

Mtanange mwingine utawakutanisha TP Mazembe dhidi ya Club Sportif Constantinois, huku FC Platinum watakuwa wanaonyesha kibarua kigumu dhidi ya E.S.T.

Timu ya Lobi Stars watacheza na Asec Mimosas huku Wydad Athletic Club watacheza na Mamelodi Sundowns.

Al Ahly Sporting Club watatoana jasho na  Jeunesse Sporting de la Saoura.

 

Advertisement