AFC Leopards ‘Ingwe’ watatii, wakaziwa uwanja

Tuesday March 3 2020

AFC Leopards ‘Ingwe’ watatii, wakaziwa uwanja,klabu ya AFC Leopards ,Mashemeji Derby,

 

By Thomas Matiko

ILE stori ya  klabu ya AFC Leopards wanaopaswa kuwa wenyeji wa Mashemeji Derby, kukaziwa uwanja wa kupigia shughuli hiyo bado ipo pale pale.

Kulingana na Mwenyekiti wa Sports Kenya, Fred Muteti, bodi iliyotwikwa majukumu ya kusimamia viwanja viwili vya kimataifa Nyayo Stadium na Moi Sports Center Kasarani, kasisitiza Ingwe watajua hawajui.

Muteti kashikilia lazima Ingwe watatii kutokana na uharibifu wa mashabiki wao walioufanyia Uwanja wa Kasarani.

Ingwe walipigwa marufuku kuutumia uwanja huo baada ya mashabiki wake kusababisha uharibifu mkubwa walipoutumia Novemba mwaka jana wakati wa mechi ya awali ya Mashemeji Derby Gor Mahia walipokuwa wenyeji.

Kulingana na Muteti, ili wakubali kuwaruhusu Ingwe kutumia uwanja huo, ni lazima walipe faini ya Sh2 milioni kwa uharibifu huo uliotekelezwa na mashabiki wao.

Lao sivyo Muteti anasema Ingwe bora watafute njia mbadala na hata kama vipi, wawazawadie Gor ana alama tatu muhimu sababu uwanja hawapewi kabla hawajalipa faini. Ni mtihani mgumu hasa ikizingatiwa kuwa Igwe wamesota  vibaya sana hivyo hata kupata tu Sh2 milioni ni taabu.

Advertisement

“Hatuwezi kuendelea kuwadekeza mashabiki wao, kama tuliwanyosha mashabiki wa Gor kuhusu uhifadhi wa viwanja vyetu hao wa AFC ndio kina nani. Watajua hawajui,” Muteti kacharuka.

Serikali iliwafungia kuitumia hadi pale watakapolipa faini ya Sh2 milioni kulipia uharibufi hiyo.

Sasa hilo ni tatizo lingine ikizingatiwa Ingwe wamesota kinoma na fedha kama hizo ni ngumu wao kuzipata.

Advertisement