Kingwendu: Taji la VPL linakwenda Yanga

Saturday September 19 2020

 

By OLIPA ASSA NA CLEZENCIA TRYPHONE

MSANII wa vichekesho nchini, Rashid Mwinshehe 'Kingwendu' amefurahishwa na kiwango kinachoonyeshwa na mastaa wa  Yanga, kinachomwaminisha kitawapa ubingwa msimu huu.
Amesema katika mechi mbili walizocheza dhidi ya Prisons ambayo walitoka nayo sare ya bao 1-1 na Mbeya City waliyoshinda bao 1-0, aliona  jinsi mastaa wa timu hiyo, wanavyocheza kwa nidhamu, mbinu na akili, jambo ambalo linamfanya atembee kifua mbele.
Amesema msimu huu utakuwa zamu ya Simba kununa, baada ya kuchukua ubingwa kwa misimu mitatu mfululizo, akijiaminisha kuwa safu yao ya ushambuliaji ipo makini hivyo inaweza kuzalisha mabao mengi zaid msimu huu.
"Yanga inashawishi kwenda uwanjani, kwani imesajili kikosi makini unaona safu ya ushambuliaji inalazimisha mashambulizi hilo linatia moyo kuona hawawezi kutoka kapa ndani ya dakika 90,"amesema Kingwendu shabiki wa Yanga lialia nakuongeza kuwa.
"Misimu mitatu ilioisha timu yetu haikuwa na kikosi kile ambacho kina wachezaji wapambanaji unaowaona wanaweza kufanya kitu katika mechi zenye ushindani wa juu, lakini msimu huu tutakuwa na kicheko, nawahamasisha mashabiki wenzangu kwenda uwanjani  kuiunga mkono timu,"amesema.
Amesema  kati ya wachezaji ambao wanamfurahisha zaidi Yanga ni Tuisila Kisinda,  Tunombe Mukoko,Micheal Sarpong, huku wazawa akimtaja Bakari Mwamnyeto na Kibwana Shomary.

Advertisement