Iringa, Mbeya na Ruvuma kila ligi wanadondosha

WAKATI ligi mbalimbali zikiwa zimesimama kwa siku kadhaa kupisha maambukizi ya virusi vya Corona, mikoa ya Kanda ya Juu imeonekana kuwa na timu vibonde zaidi kwenye kila timu.
Mikoa hiyo, Ruvuma inatimu mbili za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ambazo ni Majimaji FC na Mlale FC inaonekana imeshaaga FDL kama ilivyo kwa The Might Elephants ya Ligi Daraja la Pili (SDL) na Ruvuma Queens inayotesa Ligi Kuu ya Wanawake (SWPL).
Huko Iringa, Lipuli FC pekee inaonyesha matumaini ya kubaki TPL lakini Mtwivila FC ya SDL, Iringa United ya FDL na Panama FC Girls ya SWPL tayari hali yao mbaya.
Mkoa wa Mbeya, Timu ya Mbeya City nayo imeshaanza kuwa na mwenendo mbaya kwenye Ligi Kuu ikiwa imeshinda michezo saba kati ya 29 waliyocheza na kupotez michezo 13.
Matokeo hayo yanazifanya mikoa hiyo kushusha timu kila ligi na kufanya kuwa na idadi ndogo za timu msimu ujao kama hali hiyo itaendelea katika michezo ya mwisho.