Beka flavour: Ushindani ndiyo unaowatofautisha wasanii bora

Monday September 16 2019

Beka flavour, Mwanaspoti, Tanzania, Michezo, Muziki, Ushindani ndiyo, unaowatofautisha, wasanii bora,

 

By OLIPA ASSA

Dar es Salaam. Mwanamuziki Beka flavour amesema anazingatia nidhamu katika kazi zake ili kubakia katika ushindani wa muziki sokoni.

Beka flavour jina lake halisi Bakari Katuti alisema alisema ushindani wa hali ya juu, unaotokana na wimbi kubwa la wasanii wanaotaka kupata nafasi mbele ya jamii na wale ambao ni mastaa.

Alisema anauchukulia ushindani huo, kumjenga na kuwa kati ya wasanii ambao wataheshimika kupitia mashairi yao ambayo yatakuwa yanaigusa moja kwa moja mashabiki wao.

"Hakuna kazi rahisi hata siku moja, ili upate heshima mbele ya jamii ujue umefanya kitu ambacho kimewagusa ndicho napaswa kukifanya kwenye kazi yangu ya muziki."

 "Muziki kwangu ni kazi hivyo lazima nifanye vitu ambavyo vitafanya kazi yangu iwe ya thamani, ushindani ni mzuri kwani unaonyesha ni kiasi gani tunaweza kufikiria vitu vikubwa kwa hiyo ni vizuri ukaendelea zaidi ya hapa," alisema Beka flavour.

Advertisement