Manula aanza golini Simba kamili kuivaa UD Songo

Muktasari:

Manula ameondolewa katika kikosi cha Taifa Stars kinachojianda kwa mchezo dhidi ya Burundi

Dar es Salaam. Kipa Aishi Manula amereja katika kikosi cha kwanza Simba kitakachoanza leo dhidi ya UD Songo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Manula aliyekuwa akisumbuliwa na majeruhi kwa muda hakucheza katika mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa dhid ya UD Songo iliyofanyika Maputo, Msumbiji pamoja na mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam ambayo alidaka kipa Beno Kakolanya.

Katika mchezo huu kocha Patrick Aussems ameonyesha uaminifu wake kwa beki Gadiel Michael aliyekosa mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam.

Gadiel ameacha akichukua nafasi ya Mohamed Hussen leo ataanzia benchi, kama ilivyokuwa katika kwanza dhidi ya UD Songo jijini Maputo.

Kocha Aussems bado anaimani na wachezaji wake aliokuwa nao msimu uliopita katika kikosi cha nyota 11 watakaonza leo ni wachezaji wanne tu wapya aliopata nafasi ya kuanza.

Wachezaji hao wapya ni beki Gadiel, Deo Kanda, Sharaf Shiboub na Francis Kahata.

Kocha Aussems ameingia na mfumo wake wa 4-3-3 katika hakikisha anapata matokeo mazuri mapema katika mchezo huo.

Kikosi cha Simba: Aishi Manula, Shomari Kapombe, Gadiel Micheal, Erasto Nyoni, Pascal Wawa, Jonas Mkude, Deo Kanda, Sharaf Shiboub, Meddie Kagere, Clatous Chama na Kahata.

Akiba: Beno Kakolanya, Mohamed Hussein, Tairone Dos Santos, Mzamiru Yassin, Hassan Dilunga, Gerson Vieira, na Miraji Athuman