Mpepo amtangazia vita Lwandamina

Monday August 19 2019

Mwanasport, Mpepo amtangazia, vita Lwandamina, Yanga, Simba, Mwanaspoti,

 

KABLA ya hata kuanza kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Zambia, mshambuliaji wa Kitanzania, Eliuter Mpepo amemtangazia vita ya ubingwa Kocha wa ZESCO United, George Lwandamina.
Mpepo alisema amezungumza na Lwandamina kwenye mazingira ya utani lakini dhamira yake ni kutaka kutwaa ubingwa wa  Ligi Kuu ya Zambia ili timu yake icheze Ligi ya Mabingwa msimu ujao.
Buildcon inashiriki Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kumaliza nafasi ya tatu msimu uliopita ilipoifunga Zanaco mabao 3-1 na Mpepo akifunga mabo yote kwenye mchezo huo.
“Nilimwambia (Lwandamina) tunaweza kukutana kwenye mchezo wa fainali msimu ujao, alicheka na kuniambia anatamani tukutane ili anionyeshe kuwa yeye ndiye mwenye mpira wa Zambia.
“Hatupo ukanda mmoja ndio maana sio rahisi kukutana nao, tutakutana kama wote katika nafasi ya kwanza kwa maana ya sisi ukanda wetu na wao,” alisema Mpepo. Msimu uliopita Zesco ilitwaa ubingwa wa Ligi ya Zambia baada ya kuifunga Green Eagles kwa penalti 3-1.

Advertisement