VIDEO: Kapombe atoa neno kurejea kikosini Simba

Muktasari:

Kapombe ameanza mazoezi na wenzake katika kambi ya Afrika Kusini ameushukuru uongozi kuandaa kambi hiyo

Rostenburg. Beki wa Simba, Shomari Kapombe amesema amefurahi kupata nafasi ya kurejea katika kikosi cha mabingwa hao baada ya kuwa nje kwa nusu msimu kutokana na majeruhi.

Kapombe ameanza mazoezi na wenzake katika kambi ya Afrika Kusini ameushukuru uongozi kuandaa kambi hiyo.

"Ni jambo la kushukuru kwa kwa uongozi kutuandalia kambi kama hii kwa sababu tunapata kile ambacho tunakihitaji,"alisema Kapombe.

"Kikubwa ambacho tunawaambia mashabiki wawe na amani hiki tunachojifunza kinakwenda kutupa matokeo mazuri kwenye michezo yetu," alisema Kapombe.

Beki huyo ameweka wazi aina ya mazoezi wanayofanya yatakuwa na faida kwao ambapo sasa wanafanya ya nguvu, mbinu kidogo na ufundi.