Kambi ya Sauzi yampa mzuka kinoma Chama

Muktasari:

Ipo kambini Afrika Kusini ikijiandaa kwa tamasha la Simba Day pamoja na Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa msimu huu

Rostanburg. Kiungo wa Simba, Cletous Chama amesema maandalizi wanayofanya hapa Afrika Kusini yanampa morali ya kufanya mambo makubwa zaidi msimu huu.

Chama ambaye hachokwi kutamkwa midomoni mwa mashabiki wa Simba kutokana na kiwango chake cha juu alichoonyesha msimu uliopita.

Bao alilofunga kwa kisigino katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Nkana likaifanya Simba iingie hatua ya makundi halitasahaulika.

Alisema, hawezi kutofautisha kambi ya Afrika Kusini na Uturuki waliyokaa msimu uliopita kwa sababu kila moja ina ubora wake.

"Hii ya hapa iko tulivu, hakuna muingiliano wa watu kama kule Uturuki, imetulia na kumfanya mchezaji kushika yote anayofundishwa," alisema Chama.