Diamond: Sikusema nitafunga ndoa na Tanasha

Muktasari:

Msanii Diamond amesema watu wamemtafsiri vibaya kuwa angefunga ndoa na Tanasha kwa kuwa hakuna mahali alipotanga hivyo.

Dar es Salaam. Mwanamuziki Diamond Platnumz amesema hakuna mahali alitangaza kufunga ndoa na Tanasha.

Diamond amesema anachojua aliwaambia mashabiki zake kwamba atafanya sherehe ya kuzaliwa kwa mama na mchumba wake Tanasha.

Katika mahojiano yake leo Julai 8, 2019, Diamond alisema hiyo swali amekuwa akiulizwa mara kwa mara, lakini ukweli ni kwamba hajatangaza kufanyika kwa ndoa.

Alipoulizwa na siku ya leo aliyoiandika kwenye ukurasa wake wa wa Instagram kuwa leo angemaliza kabisa, alisema ilikuwa ni katika kupamba sherehe hizo lakini sio kwamba kuna harusi.

"Katika sherehe kina mbwembwe nyingi, nachoshukuru ni shughuli ya wapendwa wangu hawa umeenda vizuri na kuisha salama.

"Nawashukuru watu wote waliojitokeza kunipa sapoti katika kusheherekea siku hii muhimu kwangu," alisema.

Kuhusu harusi Diamond alisema siku ikifika atatangaza na kwa kuwa yeye ni mtu maarufu watu watajua tu.