Man United, Liverpool, Arsenal kuanza mbio za kuivua ubingwa Manchester City kesho

Wednesday June 12 2019

Man United, Liverpool, Arsenal, kuanza mbio za kuivua ubingwa, Manchester City kesho

 

London, England. Ratiba ya Ligi Kuu England ya msimu 2019-20 inategemewa kutangazwa kesho Alhamisi.

Mechi ya ufunguzi wa ligi hiyo itacheza Jumamosi Agosti 10 na mechi ya mwisho itachezwa Jumapili ya Mei 17, 2020.

Manchester City iliyotwaa ubingwa wa Ligi Kuu kwa tofauti ya pointi moja kwa mabingwa wa Ligi ya Mabingwa, Liverpool itakuwa na lengo la kutetea ubingwa wake kwa mara ya tatu mfululizo.

Norwich City, Sheffield United na Aston Villa zimerejea Ligi Kuu msimu huu.

Liverpool na mabingwa Europa Ligi, Chelsea watamkosa Eden Hazard aliyejiunga na Real Madrid, wakati watakapokutana  katika mchezo wa Uefa Super Cup utakaochezwa Istanbul, Uturuki siku ya Jumatano Agosti 14.

Wolves inatakiwa kucheza mechi tatu za kusaka kufuzu kwa Europa Ligi kabla ya kucheza mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu England.

Advertisement

Kwa mara ya kwanza katika historia ya Ligi Kuu England, klabu zitapata mapumziko mafupi ya wiki mbili mwezi Februari.

Kutakuwa na jumla ya mechi 380 zitakazochezwa kwa msimu mzima wa 2019-20.

Advertisement