Beki Kyata ajiweka sokoni kiaina

Sunday June 9 2019

Mwanaspoti, Michezo, Mwanasport, Beki Kyata, ajiweka, sokoni, Gor Mahia

 

By ELIYA SOLOMON

Dar es Salaam.Beki wa kati wa Mount Kenya United, Amani Kyata ameamua kuaga kwa wadau na mashabiki wa klabu hiyo mara baada ya kushuka daraja.

Kyata aliyewahi kuichezea Chemelil, alisema sababu kubwa  iliyomfanya kuondoka Mount Kenya United ni kiu  ya kutaka kukabiliana na changamoto mpya za soka sehemu nyingine.

“Naona umefika muda wa kwenda sehemu nyingine kuanza maisha mapya, nimekuwa na furaha hapa, lakini sina neno lingine zuri la kusema zaidi ya kwakheri.

“Nawatakiwa mafanikio mema. Nimejifunza vitu vingi na tumepita pamoja kwenye nyakati tofauti kwa niliowakwanza naomba wanisamehe,” alisema Kyata.

Kyata alimaliza msimu akiwa na mabao saba ambayo ni rekodi ya kuwa beki mwenye mabao mengi zaidi kwenye msimu huo, uliopita ambao Gor Mahia wameteta ubingwa wao wa KPL.

Mount Kenya United imamaliza msimu wa Ligi Kuu Kenya, ikiwa nafasi ya mwisho (18) wakiwa na pointi 18 walizojikusanyia kwenye michezo 34.

Advertisement

 

 

Advertisement