Mechi za mkwanja mrefu zilizopigwa msimu huu

Saturday May 25 2019

Mwanaspoti, Michezo, Mechi, mkwanja, Barcelona, Liverpool, Mwanasport, Michezo blog

 

London, England.MPIRA pesa unaambiwa. Kama huna pesa, basi jiandae kuteseka. Kuna jambo moja, kwa sasa thamani za wachezaji huko sokoni zimekuwa zikipanda sana, kiasi cha kuzifanya timu vigogo kuwa na vikosi vyenye thamani kubwa sana wanapoingia uwanjani kucheza mechi.
Kutokana na hilo, kuna baadhi ya mechi hizo zilichezwa msimu huu huko kwenye ligi mbalimbali za Ulaya na kushuhudia vikosi vyenye thamani kubwa sana ndani ya uwanja.
Hizi hapa mechi tano ambazo vikosi vilivyochezeshwa vilikuwa na thamani kubwa sana ndani ya uwanja na kuthibitisha mpira wa dunia ya sasa hivi, unahusu pesa tu.

5. Liverpool 2-0 Chelsea - Euro 1.31 bilioni
Liverpool walikuwa nyumbani Anfield kucheza na Chelsea katika mchezo wa Ligi Kuu England, Aprili 14. Mchezo huo, Liverpool walishinda 2-0 na kurudi kwenye matumaini yao ya kubeba ubingwa. Kwenye mchezo huo, Liverpool walianzisha kikosi kilichokuwa na thamani kubwa sana ndani ya uwanja kilichokuwa na wakali kama Alisson Becker na Virgil van Dijk na kufanya thamani ya Euro 713 milioni, wakati Chelsea wao kikosi chao kwenye mechi hiyo kilikuwa na thamani ya Euro 598 milioni.

4. Man City 6-0 Chelsea - Euro 1.34 bilioni
Kichapo kingine cha Chelsea kwa msimu huu kilihusisha mechi iliyokuwa na vikosi vyenye thamani kubwa sana ndani ya uwanja. Chelsea waliwakabili Manchester City katika mchezo ambao vikosi vilivyocheza vilikuwa na thamani ya Euro 1.34 bilioni. Mechi hiyo iliyopigwa Etihad, Chelsea alichapwa 6-0, huku Man City walikuwa na kikosi chenye thamani ya Euro 710 milioni uwanjani, wakati Chelsea walikuwa na kikosi chennye thamani ya Euro 625 milioni na kufanya kuwa moja ya mechi yenye thamani kubwa kwenye msimu.

3. Barcelona 3-0 Liverpool - Euro 1.40 bilioni
Barcelona na Liverpool zilikutana kwenye robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu, ambapo mechi ya kwanza ilipigwa uwanjani Nou Camp na wenyeji kushinda 3-0.
Kwenye mchezo huo, timu hizo zilimennyana jino kwa jino na hata ule wa marudiano uliofanyika Anfield, ambapo Liverpool ilishinda 4-0.
Lakini, kwenye ile mechi ya kwanza, vikosi vilivyokuwa uwanjani vilikuwa na thamani ya Euro 1.40 bilioni.
Barca iliingiza kikosi chenye thamani ya Euro 758 milioni, wakati Liverpool ilikuwa na thamani ya Euro 645 milioni.

2. Real Madrid 0-1 Barcelona - Euro 1.43 bilioni
Mechi ya El Clasico ni jambo la kawaida kuhusisha masupastaa wa nguvu ndani ya uwanja. Kitu cha kushangaza imekuwa mechi ya pili kwenye orodha hii ya mechi zilizokuwa na thamani kubwa sana uwanjani wakati inachezwa kutokana na thamani za vikosi.
Mechi hiyo ilimalizika kwa Barcelona kushinda 1-0. Uwanjani hapo, Real Madrid kikosi chake kilikuwa na thamani ya Euro 605 milioni, wakati kile cha Barca kwenye mechi hiyo walichezesha kikosi kilichokuwa na thamani ya Euro 820 milioni.

1. Barcelona 2-0 Atletico Madrid - Euro 1.46 bilioni
Barcelona imehusika tena kwenye mechi yenye thamanni kubwa zaidi uwanjani wakati walipowakabili wapinzani wao Atletico Madrid huko kwenye La Liga mwezi uliopita. Barca ikiwa nyumbani ilishinda 2-0 na ilikuwa na kikosi chenye thamani kubwa pia ndani ya uwanja.
Kwenye mechi hiyo,

Advertisement