Kumbe sio Simbu tu! kuna wengine

Thursday May 16 2019

 

By Imani Makongoro

KOCHA aliyemuibua mwanariadha nyota wa Timu ya Taifa, Alphonce Simbu, Jambau Madai ana rekodi tamu sana kwenye riadha.

Jamaa mbali na Simbu amewaibua nyota wengine 25, ambao 13 kati ya hao wako jeshini kutokana na na vipaji vyao huku wengi wao wakiwa ni tegemeo kwenye kikosi cha timu ya Taifa.

Jambau ambaye mwaka huu alipewa nafasi ya kuwa kocha msaidizi wa timu ya Taifa iliyoshiriki mbio za nyika za dunia, amemuibua pia Samson Ramadhan, Faraja Lazaro na Jackline Sakilu ambao wapo timu ya JWTZ.

Wanariadha wengine walioibuliwa na kocha huyo ni Maria Misanga, Nasra Hambu, Nasra Ally, Elizabeth Ivonis, Fanesta Mbugha, Paskal Ntui, Marco Monko, Nestory Huda na John Joseph.

Wengine ni Dorcus Boniface, Said Makula, Agnes Protas, Daniel Sinda, Rozalia Fabiano, Mohamed Mbua, Bakari Jumanne, Angelina Itambu, Epmack Boniface, Samwel Makiya na Jonas Gwae.

Katibu Mkuu wa Riadha Tanzania, Wilhelm Gidabuday alisema kocha huyo amekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya mchezo huo na ndiyo sababu waliamua kumtumia kwenye Timu ya Taifa ya Nyika.

Advertisement

Advertisement