Hii kali! Uchaguzi Yanga umemgusa hadi Rage aisee

Friday April 12 2019

Mwanasport, Mwanaspoti, Uchaguzi, Yanga, Rage, Simba v TP Mazembe, Makambo, Manji, Kagere, Boccoee

 

By IMANI MAKONGORO

Dar es Salaam. Hakuna utani wa jadi bila Yanga Imara au Simba imara na hilo limeonwa na Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage ambaye ametia neno kuelekea kwenyue uchaguzi wa watani wake, Yanga.
Yanga ambayo imetetereka kiuchumi itafanya uchaguzi Mei 5 kupata mwenyekiti mpya wa klabu sanjari na makamu mwenyekiti na wajumbe wa kamati ya utendaji.
Wakati Yanga ikielekea kupata viongozi wapya, Rage amewashauri wanachama kuchagua kiongozi mwenye mipango ya kuindesha klabu yao kisasa.
"Yanga sio maadui zetu ni watani zetu, bila shaka wanajua kiongozi wanayemtaka," alisema Rage na kuendelea.
"Hapa nchini watu wanaotaka umaarufu uwa wanakimbilia klabu za Simba na Yanga, hivyo watani zangu Yanga waliangalie hilo kwa uzito Mei 5, ili tutakapokuwa tukiwafunga wasije kusingizia uongozi haupo," alimaliza Rage kwa utani.

Advertisement