Kumekucha Uchaguzi Yanga Mei 5, fomu kutolewa kesho Jangwani

Muktasari:

Yanga kwa kushirikiana na TFF watafanya uchaguzi mkuu Mei 5, fomu zitaanza kupatikana kesho makao makuu ya klabu hiyo pale Jangwani.

Dar es Salaam. Yanga itafanya uchaguzi wa mkuu, Mei 5 baada ya kamati yao kukubaliana kushirikiana na Shirikisho la Soka Tanzania 'TFF'.

Samuel Mapande mwenyekiti wa kamati ya Yanga pia ni wakali wa klabu hiyo, amesema wapo tayari kufanya uchaguzi kwa kushirikiana na TFF.

"Yanga tupo tayari kufanya uchaguzi mkuu na ndio maana tupo hapa kuujulisha umma wa Watanzania" anasema.

Mwenyekiti wa uchaguzi TFF, Ally Mchungahela alitangaza tarehe ya uchaguzi na kwamba fomu zitaanza kutolewa kesho Jumanne katika makao makuu ya klabu ya Yanga.

"Yanga wanahitaji uchaguzi huru ndio maana tumekubaliana tushirikiane na fomu zichukuliwe kwenye klabu yao kuanza kesho Aprili 2-7, 2019.

"Wale ambao walichuku   mwanzo hao hawana haja ya kuchukua tena watasubiri mchakato wa kuungana na wenzao ambao watapita kwenye mchakato huo" anasema.

Mchungahela amewata Wanayanga kuondoa hofu kwa madai reja za Yanga zimekabidhiwa TFF ili kuhakikisha mchakato huo unakwenda vizuri na kwa haki.

"Ndio maana viongozi ambao walikuwepo Yanga wamejiuzuru ili kupisha uchaguzi mkuu ufanyike, reja tunazo tutawaacha wawe huru TFF itasimamia tu" anasema.