Samatta apiga moja, Genk yaloa 3-1

Muktasari:

Samata anakuwa mtanzania wa kwanza kufunga mabao 20, katika Ligi Kuu Ubelgiji

Ubelgiji. Mshambuliaji Mbwana Samatta amefunga bao moja wakati timu yake ya Genk ikikubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka Clubb Brugge katika mchezo wa Ligi Kuu Ubelgiji.

Samatta alifunga bao hilo pekee katika dakika 77, akiunganisha kwa kichwa mpira wa kona na kumfanya nahodha huyo wa Taifa Stars kufikisha idadi ya mabao 20 msimu huu.

Pamoja na kipigo hicho Genk inaendelea kuongoza ligi ikiwa na pointi 57 ikifuatiwa na Club Brugge (49) huku Standard Liege ikiwa ya tatu na pointi 46.

Katika mchezo huo mabao ya Brugge yalifungwa na Clinton Mata katika dakika 21, kabla ya Siebe Schrijvers kuongeza la pili na Ruud Vormer kuongeza la tatu.