Muumin, Bakule wafanya shoo barabarani

Saturday December 8 2018

 

By Charles Abel

Wanamuziki Rogart Hega 'Caterpillar', Khadija Mnoga 'Kimobitel', Mwinjuma Muumin na Badi Bakule wamegeuka kivutio jijini leo baada ya kubuni staili ya kufanya shoo hadi barabarani.
Staili hiyo mpya na ngeni katika muziki wa dansi imeibuka leo Buza jijini Dar es Salaam ambako wanamuziki hao walikuwa na shoo ya kutumbuiza kwenye bonanza maalum la soka lililoshirikisha timu nne za Mavererani.
Muumin, Bakule, Kimobitel, Hega pamoja na madansa wao ambao walikuwa wanaimba nyimbo zao zilizowahi kutikisa nchini, waliwainua watu vitini baada ya kutoka jukwaani na kuelekea kwenye barabara ya Buza na kuanza kucheza.

Advertisement