KCCA, Mtibwa Sugar kupigwa Desemba 15

Thursday December 6 2018

 

Kampala, Uganda. KCCA imethibisha Desemba 15 ndiyo siku watakayocheza mechi yao ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Mtibwa Sugar.

Mtibwa Sugar imewatoa Northern Dynamo kwa jumla ya  mabao 5-0 katika raundi ya awali na kupata tiketi yakucheza dhidi ya KCCA mabingwa wa Kombe la Stanbic Uganda.

KCCA ilipata nafasi ya kuanzia hatua hiyo baada ya kufanya vizuri katika mashindano ya Afrika kwa miaka miwili mfululizo iliyopita.

KCCA mechi ya kwanza itachezwa Lugogo na marudiano wiki moja baadaye yatafanyika Dar es Salaam.

Mshindi wa jumla wa mechi hiyo Mtibwa na KCCA atasubili kucheza na moja ya timu zilizotolewa katika raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Advertisement