Kesi ya Malinzi kunguruma Jumatano, Alhamisi hii

Muktasari:

Kesi inayomkabili, aliyekuwa rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Jamal Malinzi na wenzake wa wanne itandelea kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ushahidi wa upande wa mashtaka Novemba 21 na 22 mwaka huu.

Dar es  Salaam. Kesi inayomkabili, aliyekuwa rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na wenzake wa wanne itaendelea kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka, Novemba 21 na 22, mwaka.
Kesi hiyo Leo,  Novemba 15, ilipangwa kwa ajili ya kutajwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri na kwamba itaendelea kusikilizwa ndani ya siku hizo mbili mfululizo.
 Katika kesi hiyo, ipo katika hatua ya kutolewa kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka na shahidi wa nane ambaye ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Kidao Wilfred (41) ndiyo anaendelea kutoa ushahidi wake.
Washtakiwa katika kesi hiyo mbali na aliyekuwa rais TFF, Jamal  Malinzi(57) wengine ni Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine(46) na Mhasibu wa TFF,  Nsiande Isawayo(27).
Meneja wa  Ofisi TFF, Miriam Zayumba na Karani wa TFF, Flora Rauya ambao Kwa pamoja  wanakabiliwa na mashtaka 30 katika   kesi ya jinai namba 213 ya mwaka 2017 yakiwamo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha wa USD 173,335 na Sh 43,100,000.
Malinzi, Mwesigwa na Nsiande wapo rumande kwa kukabiliwa na mashtaka ya utakatishaji wa fedha kuwa miongoni mwa mashtaka  ambayo kwa mujibu wa sheria hayana dhamana huku wenzao Zayumba na Frola wapo nje kwa dhamana.