Kipigo bado chamuumiza Ronaldo

Saturday November 10 2018

 

Turin, Italia.INAONEKANA kama Cristiano Ronaldo bado haamioni kama Manchester United inaweza kuilaza Juventus, lakini hali haiendani na anavyodhani.
Katika mechi ya Ligi ya Mabingwa, Manchester United iliilaza timu hiyo mabaop 2-1 katika mechi iliyokuwa kali na kusisimua huku Red Devils ikipambana kwelikweli na kuibandua Juventus.
Ronaldo aliyekuwa amepania kuwatungua 'jamaa' zake, alishuhudia timu yake ikilala kwa bao la kujifunga la Alex Sandro lililoipa jeuri timu hiyo ya England.
‘Nilifurahi kupata mabao ya mapema, lakini iliniboa tuliporuhusu mabao tena ya kujifunga. Mchezo ule ilikuwa tushinde mabao matatu hadi manne kwa kuwa tuliutawala,’ Ronaldo alisema akiizungumzia mechi ya Manchester..
Aliifungia timu yake kwa mpira wa frikiki kupitia kwa Juan Mata kabla krosi ya Ashley Young kumbabatiza Sandro dakika za lalasalama na kujaa wavuni huku Ronaldo akifunga bao lake la kwanza la Ligi ya Mabingwa akiwa na Juventus.

Advertisement