#UCHAGUZI SIMBA: Dalali anachotaka pointi tatu tu kila mechi

Muktasari:

Dalali anashikiria rekodi ya kutopoteza mchezo wowote wa Ligi Kuu chini ya uongozi wake mwaka 2010.

Dar es Salaam. Wakati zoezi la kuhesabu kura za wanachama wa Simba waliopiga kuchagua wajumbe na mwenyekiti watakaowaongoza kwa miaka minne ijayo mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassan Dalali amesema, mshindi yeyote atakayechaguliwa anachotaka ni pointi tatu za kila mechi.

Uchaguzi Mkuu wa Simba umefanyika leo Jumapili kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere wa kupata viongozi wapya wa kuiongoza klabu hiyo kwa miaka minne ijayo.

Dalali amesema: "Kwangu mimi mtu yeyote sera kubwa ni pointi tatu. Wamejieleza kwangu ninachoangalia ni ushindi wa kila mechi."

Dalali amesema, pamoja na mambo yote watu wanataka furaha kwa sababu ndiyo kila kitu.