Rasta Jaffary aanza na bao Yanga

Muktasari:

Kiungo Jaffary Mohammed ndio mchezo wake wa kwanza ligi kuu tangu asajiliwe na kikosi cha Yanga

Dar es Salaam.Kiungo Yanga, Jaffar Mohammed ameanza kwa kishindo baada ya kufunga bao katika mchezo wake wa kwanza tangu ajiunge na mabingwa hao wa kihistoria.

Rasta Jaffar alifungia Yanga bao la kusawazisha akiunganisha kwa kichwa krosi ya Ibrahimu Ajibu kufuta bao la mapema lililofungwa na Ndanda.

Jaffary ambaye alisajiliwa na kikosi hicho akitokea katika kikosi cha Majimaji, hajawahi kuichezea timu hiyo mchezo wowote wa Ligi Kuu.

Katika mchezo huu alikuwa anacheza kama mshambuliaji wa pili nyuma ya Herieter Makambo, huku Ibrahim Ajib akitokea kwa chini.

Katika upande wa kiungo walikuwa wanacheza Feisal Salum na Maka Edward katika eneo hilo wakisaidiwa na Ajib aliyekuwa anacheza juu yao.

Pacha ya Jaffary na Makambo ilikuwa inaonekana haina spidi ya kutosha kwani wote walikuwa wakijivuta katika kupeleka mashambulizi.