#UCHAGUZI SIMBA:Kagere auteka mkutano mkuu Simba

Muktasari:

Simba msimu huu itashiriki mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza baada ya kuwa nje za kwa zaidi ya miaka mitano

Dar es Salaam.Mshambuliaji Medie Kagere amekuwa mchezaji wa kwanza kutamkwa kwenye mkutano mkuu wa Simba unaoendelea jijini.

Kagere alitamkwa na Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara akiwambia wanachama waliofurika ukumbi wa JNICC kuwa wachangamke kwani Simba siyo timu ya mchezo mchezo.

"Kagere anawakimbiza tu huko uwanjani, halafu mnakuwaje wanyonge embu changamkeni bwana," alisema Manara huku akikokeza kauli yake kwa kutamka kauli mbiu ya Simbaaa, na wanachama kuitikia kwa nguvu wakishangilia, Nguvu moja.