#UCHAGUZI SIMBA:Hassanoo aamsha shangwe ukumbini

Muktasari:

Hassanoo amewahi pia kushika nyadhifa mbalimbali ndani ya Simba ikiwemo Kamati ya Usajili. Pia alikuwa mwenyekiti wa Chama cha Soka Pwani.

Dar es Salaam. Hassan Hassanoo ameamsha shangwe kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere baada ya kitambulishwa.

Hassanoo ambaye aliwahi kuwa makamu mwenyekiti wa Simba amehudhuria mkutano wa leo wa Uchaguzi mkuu wa klabu hiyo.

Haji Manara alikuwa akitambulisha watu mbalimbali maarufu na wanachama kupiga makofi, lakini alipofika kwa Hassanoo alimtambulisha na kuchombeza kuwa mpiganaji na wanachama walilipuka kwa makofi mengi zaidi.