Tandale wamuamuru Jackline Mengi avue miwani

Friday October 5 2018

 

By Nasra Abdallah

Wakazi wa Tandale wamejikuta wakimpa wakati mgumu mke wa mfanyabiashara maarufu nchini Reginald Mengi.
Jackline Mengi aliamriwa avue miwani ili wamuone akiongea. Hali hiyo imemfika baada ya kusimama kuwasalkmia ikiwa ni muda mfupi tangu afike hapo.
Alipoanza kuongea, wakazi hao walisikika wakisema"vuaaaaa" alipouliza nini,wakamjibu via miwani hiyo.
Baada ya kuivua na kuwaangalia,aliwauliza mmeridhika mnaniruhusu nivaw sasa wakamjibu"ndioooo" kisha wakaanza kumsikiliza kwa utulivu.
Katika ujumbe wake, Jacline maarufu kwa jina la Keylin amewataka kina mama watakaopata mitaji kutoka kwa Diamond waitumie kama ilivyokusuduwa
"Wakina mama nawaambia hela ya mtaju hailiwi na nyie kina baba msiwabe wakina mama hizo hela,acheni wafanye biashara," amesema Kyllne.
 Kwa upande wake,
Babu Tale amesema hajawahi kufikiria kama  angewahi kufika Tandale.
Amesema amefurahi kwa kuwa hiyo yote ni katika kumuunga mkono msanii wao Diamond.
"Nashukuru pia Jacline amebkambia amekuwa akija kufanya manunuzi ya vyakula mbalimbali hapa Tandale,hivyo huyu ni mwenzetu.

Advertisement