Bocco, Kapombe ni mwendo wa kuchati tu jukwaani!

Arusha: Nahodha wa timu ya Sc John Bocco pamoja na beki Shomari Kabombe wameendelea kuwa benchi ya timu hiyo baada ya kuonekana jukwaani wakati timu yao ikishuka dimbani kucheza na Arusha United.
Bocco hajaoneka uwanjani tangu timu hiyo ilipotoka nchini Uturuki walipoweka kambi kwa siku kadhaa wakijiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Barua.
Hata hivyo katika mkutano na waandishi wa habari alikiri kuwepo kwa ushindani wa namba kwenye timu hiyo baada ya usajili kufanyika.
Aliongeza kuwa kila kukicha wachezaji wanakuja wapya na wenye uwezo tofauti kwenye timu, hivyo lazima mchezaji afanye mambo ya ziada ili kumfurahisha kocha kumpatia nafasi ya kucheza.