Mpira Pesa waja kivingine Simba Day

Wednesday August 8 2018

 

Tawi la Mpira Pesa linaloongozwa na Mwenyekiti wake, Ostadhi Masoud katika wiki ya Simba wao wamefanya matukio makubwa mawili ambayo yote yamehusisha shughuli za kijamii.

Masoud alisema kwa ukubwa wa tawi lao Ijumaa walikwenda katika kituo kimoja cha watoto yatima kilichopo Tabata Dar es Salaam na waliwapatia unga wa ngano kilogramu 25 viroba vitatu, mafuta ya kupikia kindoo kimoja na Sukari kilogramu 15.

"Baada ya matokeo hayo walimekubaliana kwa pamoja kwenda katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutoa damu kwa kuwapatia wahitaji," alisema Masoud.

Advertisement